Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 7:30 am

NEWS;WAKURUGENZI WAPEWA RUNGU KUAJIRI WAFAMASIA.

BUNGENI DODOMA; Serikali imewaruhusu wakurugenzi wa halmashauri zenye uwezo kuajiri kwa mkataba wamafasia na mteknolojia wa dawa msaidizi kwa kuwalipa kupitia kwenye mapato yao ndani ili kuondokana na changamoto uhaba wa watalaam hao.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 7, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bukene Selemani Zedi(CCM).

Katika swali lake, Mbunge huyo amehoji, serikali kama haioni umuhimu wa kuruhusu waganga wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuajiri wataalam hao kwa mkataba wa muda wakati wanasubiri ajira.

Aidha, alisema wakati mwingine wananchi wanaenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wanakosa dawa sio kama dawa hizo hazipo MSD, bali ni matatizo ya uagizaji yanayotokana na vituo vya afya kutokuwa na watu hao muhimu.

Akijibu swali hilo, Dokta Dugange amesema tayari walishatoa maelekezo kwa wakurugenzi ambao halmashauri zao zina uwezo wa mapato ya ndani kuajiri kwam ikataba wataalam hao ili waweze kuajiriwa.

Amesema kuwa wataalam hao wakiajiriwa kwa mkataba wasimamiwe kwa karibu na waganga wakuu wa wilaya ili kuhakikisha huduma hizi za upatikanaji wa dawa katika vituo zinaboreshwa huku akimhakikishia mbunge huyo kuwa jambo hili limeshafanyiwa kazi na serikali.

Aidha, ametoa wito kwa wakurugenzi wote wa mamlaka za serikali za mitaa nchini kutumia fursa hiyo kwa wale wenye uwezo wa kuajiri.