- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS;VIJIJI VYOTE VYA SINGIDA MASHARIKI KUPATA UMEME NDANI YA MIEZI 18.
DODOMA; Serikali imeahidi kufikisha umeme katika vijiji vyote vilivyopo Tarafa ya Mung'haa Jimbo la Singida Mashariki ndani ya kipindi Cha miezi 18 kuanzia Mei 28,2021.
Ahadi hiyo imetolewa Mei 29,2021,na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akiongezea majibu kwenye swali la nyongeza la Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu.
Katika maswali yake Mtaturu ametaka kujua ni lini mkandarasi atakwenda kuanza kazi.
"Nataka kujua hususan Tarafa ya Mung'haa ambayo ina kata Saba haina umeme kabisa,na Kama ulivyosema tangu mwezi Machi lakini mpaka sasa hajapatikana na tunataka kujua jina la mkandarasi huyo na lini atakwenda," alihoji Mtaturu.
Aidha amehoji pia Kama serikali haioni sababu ya kuongeza Kasi ya kuweka umeme katika vitongoji vilivyobaki kutokana na mradi wa ujazilishaji lakini unaenda taratibu.
Akijibu maswali hayo Dkt Kalemani amekiri kuwa ni kweli Jimbo la Mtaturu kuna Tarafa ambayo haijapata umeme ila wakandarasi tayari wameondoka kwenda Singida kufanya kazi ikiwemo na kwenye Tarafa hiyo.
"Mtaturu alikuwa na vijiji 12 ambavyo havijaguswa kabisa pamoja na hiyo tarafa,nimhakikishie yeye pamoja na madiwani na wananchi katika Jimbo lake wote watapata umeme ndani ya miezi 18 kuanzia jana tulipopeleka wakandarasi,"alisema Kalemani.