- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS:DKT. GWAJIMA AWATAKA WAKURUGENZI WA TAASISI KUAINISHA CHANGAMOTO NA MAHITAJI ILI KUTEKELEZA ILANI.
DODOMA: Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametakiwa kuanisha changamoto na mahitaji yote yanayohitajika ili kuakisi na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuwezesha kuleta maendeleo katika sekta ya afya nchini.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Dorothy Gwajima wakati wa majumuisho ya kikao kazi cha wakurugenzi wa wizara na taasisi zake waliokutana jijini Dodoma na kujadili hali ya utoaji huduma za afya nchini.
Dkt. Gwajima amesema kuwa licha ya maelekezo mengi ambayo yamekwishatolewa kazi kubwa ambayo wanatakiwa kufanya ni kuandaa vibango kitita vya changamoto zote walizonazo katika taasisi zao na namna gani wanaweza kuzitatua katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
“Mnapoondoka hapa mnajua tunazo kazi za kufanya, mkaweke changamoto zenu katika madaraja na kuainisha ni changamoto zipi sisi tunatakiwa kuhusika na zipi nyinyi na taasisi zenu mnatakiwa kuhusika na nini kifanyike na kwa njia zipi kwa kujumuisha Ilani kwa mwaka wa kwanza hadi wa tano”. Alisisitiza Dkt. Gwajima.
Aidha, Waziri huyo aliwataka wakurugenzi hao kutokukaa na changamoto bali wanapaswa kufanya vitu kuendana na muelekeo wa sasa ili kuleta faida na tija kwa Taifa husuani kwenye sekta ya afya.
“Ni lazima tuakisi hayo ambayo kielimu na kiuwezo tumeyafikia kwa kuzingatia dhana nzima ya Mikakati ya utekelezaji wa sera ya afya, Mkakati watano wa sekta ya afya, Mkakati wa kufikisha afya kwa wote pamoja na maeneo ya kipaumbele ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika sekta ya afya”. Aliongeza Dkt. Gwajima.
Pia Alisema kuwa ili kuweza kutekeleza hayo kwa ufanisi mkubwa Wizara yake inataka kuwa na uratibu anuwai kwa kila mkurugenzi wa taasisi kuwasilisha uelekeo wake na kufunga nao mkataba ili kuweka mazingira rafiki kwa kufikia na kutekeleza Ilani.
Wakati huo huo Naibu Waziri Dkt. Godwin Mollel amesema kikao hicho kimelenga kufahamiana na kuwa timu moja katika uwajibikaji na namna gani wanakwenda kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika sekta ya afya nchini.
Amesema kukaa kwa pamoja kunasaidia kupanga na kufanya maamuzi yaliyo sahihi ili kuweza kuwatumikia wananchi kwa pamoja na ndio maana wananchi wameiamini serikali hii hivyo timu waliyonayo ni nzuri na wataweza kufanya kazi kubwa zaidi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.