Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:31 pm

NEWS: ZITTO NA MSAJILI WATUNISHIANA MISULI

Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi ameonesha kutofurahishwa na kitendo cha kituo cha Demokrasia nchini(TCD) kupanga tarehe ya mkutano wake wa amani utakao hudhuriwa na Rais sawa na tarehe ya mkutano wa Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa utakao kutanisha Jeshi la polisi na vyama vya siasa nchini.

Jaji Mutungi aliitisha kikao cha vyama hivyo na Jeshi la Polisi alioupanga ufanyike Oktoba 21, mwaka huu ambayo ni tarehe sawa na tarehe ya Mkutano wa TCD unaokusudiwa kufanyika Oktoba 21 na 22.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi Jaji Mutungi alisema hataki malumbano na kituo hicho, kwani yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuitisha kikao hicho.

“TCD wametangaza siku ya kufanya mkutano huo baada ya kusikia mimi nimeshapanga hivyo, kama waliona kuna hali hiyo walitakiwa waandike barua au kuja ofisini kuhusu utaratibu ulipangwa na kuona tunafanyaje,” alisema Jaji Mutungi.

“Wasipohudhuria sawa kwa sababu sio mara ya kwanza kusema hivyo. Vyama viko 19 hata vikikataa vyama vitatu kwa sababu zao zingine,” alisema Mutungi.

Kwa upande wake, jana, Zitto amemwandikia barua Msajili akimtaka kutafakari upya siku aliyoitisha mkutano na vyama vya siasa na Polisi ili kuondoa mgongano wa tarehe.

“Tumewaalika viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, na taasisi zisizo za kiserikali, kwa hiyo mkutano wa TCD ni muhimu zaidi na vyama wanachama wanaupa kipaumbele,” alisema Zitto.