- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO NA MBATIA WALAANI KUSHIKILIWA KWA MBOWE
Dar es salaam. Kiongozi mkuu wa ACTwazalendo Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Francis Mbatia kwa pamoja wamelaani vikali tukio la Jeshi la Polisi nchini kuwashikilia viongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kutokana na kuratibu Kongamano la Katiba mpya.
Viongozi hao wawali wametoa wito kwa Jeshi hilo kuwaachilia Mara moja kwa viongozi hao, "kwani Haki ya kukusanyika inalindwa na katiba ya Jamhuri ya Tanzania chini ya Ibara ya 20 (1) na sheria ya vyama vya Siasa kifungu cha 11" imesema sehemu ya Tamko lilotolewa hii leo Julai 23.7.2021
Aidha wabunge hao wawali wa zamani wamewataka Raia wengine wenye mapenzi mema na nchi kukemea halii kwasababu hali hiyo inafifiza utengamano wa nchi.
Jana Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema Bw. Mbowe, anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.
Kauli hiyo imekuja baada ya kiongozi huyo wa upinzani kuwa anashikiliwa kwa takribani siku mbili, vyombo vya habari vimeripoti.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwamba, Mbowe alikamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza, jambo ambalo si kweli.
“Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika.
Hatua hiyo imefikiwa sasa,” alisema Misime.
Hivi karibuni Mbowe alifanya mkutano na waandishi wa habari na alikosoa kukamatwa kwa wafuasi wa chama hicho na polisi, pamoja na suala la mabadiliko ya katiba.