- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ZITTO, MBOWE WAPEWA TENA TAREHE YA KURIPOTI POLISI
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania (Chadema), Freeman Mbowe na kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe sambamba na wajumbe wengine watatu wa kamati kuu ya Chadema leo hii wameripoti tena kituo cha Polisi Oysterbay Jiji Dar es salaam.
Viongozi hao wa vyama vya upinzani wametakiwa kuripoti tena kituo hicho cha polisi Novemba 9, mwaka huu.
Wajumbe wengine walioripoti leo ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) Halima Mdee na waliokuwa wagombea ubunge wa Ubungo na Kawe, Boniface Jacob na Godbless Lema.
Mbowe, Lema na Jacob walikamatwa na polisi Novemba Mosi, 2020 katika kikao huku Zitto akikamatwa Novemba 3, 2020 katika kituo cha polisi Oysterbay alikokwenda kuwajulia hali wenzake. Wote waliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti leo.
Mdee alijisalimisha polisi jana baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kumtaka kuripoti kwa mahojiano.
Leo viongozi hao waliwasili kituoni hapo kwa nyakati tofauti na kuelekea kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi na ilipofika saa 4:30 walitoka kwa pamoja