Home | Terms & Conditions | Help

April 6, 2025, 7:32 am

NEWS: ZITTO AGOMA KUSAFIRISHA NA POLISI BAADA YA KUKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda ya Kusini mwa Tanzania mchana wa leo lememkamata Kiongzoi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto kabwe na Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Selemani Bungala maarufu kama Bwege na wengine nane, baada ya Jeshi hilo kuvamia mkutano wa ndani wa wanachama wa chama cha ACT- Wazalendo, uliotarajiwa kufanyika leo Juni 23, 2020 katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Baada ya kukamatwa kwa Zitto na Wenzake walipelekwa mpaka kituo cha polisi cha kilwa na Baadaye Majira ya Saa 2 usiku Jeshi hilo likatoa amri ya viongozi hao kupelekwa Mkoani Lindi na Gari la wazi, hatua ambayo Zitto aliikataa kwasababu inahatarisha maisha yao.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini aliwaambia kuwa kama mnataka kutusafirisha kwa gari hilo ni vyema watumia magari ya chama chao cha ACT Wazalendo ili kuhakikisha wanakuwa salama, hatua ambayo Polisi hawakukubaliana nalo na kulazimika kumbakiza mahabusu.

Zitto ana ziara ya siku tatu kusini mwa Tanzania, kutembelea majimbo mbalimbali anapokea madiwani wanaotaka kujiunga na chama chake ambao wamemaliza muda wao.

''Jana alikuwa katika jimbo la Rufiji na alipokea madiwani wanne kwa kikao cha ndani, leo alikuwa katika jimbo la Kilwa Kusini ambako alienda kumpeleka mbunge Suleiman Bungara maarufu Bwege ambaye hivi karibuni alijiunga na chama chetu na madiwani wanane wa chama cha wananchi CUF ambao nao wamejiunga walikuwa wanatarajiwa kupokelewa leo kwa kutumia kikao cha ndani ambao ni taratibu za kawaida za chama''. Amesema Katibu Mkuu Act Wazalendo Ado wakati akiongea na Shirika la Utangazaji la uingereza BBC.


Kiongozi huyo amelaumu kuwa Jeshi hilo linafanya vitendo hivyo kwa manufaa ya serikali iliyo madarakani badala ya kutumika kwa maslahi ya Umma.

Amesema kuwa pamoja na tukio hilo chama cha ACT Wazalendo kitaendelea na ratiba zake kama ilivyo kawaida yake kwa mujibu wa sheria, kwa kuwa chama kina uhuru wa kuendelea na shughuli za kisiasa.

Akizungumzia kuhusu matukio mbalimbali yanayojitokeza nyakati mbalimbali za uchaguzi, ado amesema '' kuna matendo kadha wa kadha ambayo yanaondosha dhana nzima ya demokrasia nchini '' akionya kuwa hawatakubali iwapo mamlaka hazitazingatia misingi ya haki na Demokrasia. ''Tutarudi kwa Umma na kuhakikisha tunasimama nao ili haki yetu ipatikane''.