Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 11:42 pm

NEWS: ZANZIBAR YALEGEZA MASHARTI YA KUKABILIANA NA JANGA LA CORONA

Zanzibar waeleza wagonjwa wapya walivyoanza kuumwa | East Africa ...

TAARIFA RASMI YA SERIKALI KUHUSIANA NA KUREGEZA BAADHI YA MASHARTI KATIKA KUKABILIANA NA MRIPUKO WA COVID-19 ZANZIBAR, TAREHE 27 MEI, 2020

NDUGU WANANCHI,

KWANZA KABISA HATUNA BUDI KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUTUJAALIA UZIMA NA AFYA NJEMA NA KUWEZA KUTIMIZA MOJA KATI YA NGUZO ZA KIISLAMU YA KUFUNGA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI, KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDDI EL-FITRI PAMOJA NA KUINGIA KATIKA MWEZI WA SHAWAL NA KWA WALE WANAOENDELEA NA FUNGA YA SITA NAWATAKIA FUNGA NJEMA.

NDUGU WANANCHI,

BAADA YA SERIKIALI KUFANIKIWA KUKABILIANA KWA KIASI KIKUBWA NA MRIPUKO WA COVID – 19, SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INACHUKUA UAMUZI WA KUREGEZA BAADHI YA MAMBO TULIYOKUWA TUMEAMUA HAPO AWALI KAMA IFUATAVYO:-

1.SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAUNGANA NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHAKIKISHA KUWA KUANZIA TAREHE 01 JUNI, 2020 VYUO VYOTE VYA ELIMU YA JUU VITAFUNGULIWA NA KUENDELEA NA PROGRAMAU ZAO KAMA KAWAIDA KWA UPANDE WA ZANZIBAR

2.WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA NAO WATAANZA MASOMO YAO TAREHE 01 JUNI, 2020 ILI KUWAWEZESHA KUFANYA MITIHANI YAO YA TAIFA. KUFUATIA MAAMUZI HAYA SERIKALI IMEIAGIZA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU NA WIZARA YA AFYA KATIKA KUANDAA MIONGOZO YA KIAFYA ITAKAYOPASWA KUZINGATIWA ILI KUEPUKA MAAMBUKIZO YA MARADHI HAYA.

3.KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA HADI CHA TANO PAMOJA NA WANAFUNZI WA SKULI ZA MSINGI, MAANDALIZI NA MADRASA, SKULI NA VYUO VYAO ZITAENDELEA KUFUNGWA HADI YATAKAPOTOLEWA MAELEKEZO MENGINE YA SERIKALI.

4.KWA UPANDE WA MICHEZO, LIGI KUU YA MPIRA WA MIGUU ZANZIBAR ITAENDELEA KUANZIA TAREHE 5 JUNI, 2020 NA TUMEIAGIZA WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO KWA KUSHIRIKIANA NA ZFF PAMOJA NA WIZARA YA AFYA KUANDAA MUONGOZO NA NAMNA BORA YA KUENDESHA LIGI HIYO.

5.KWA UPANDE WA MICHEZO MENGINE YOTE INAYOCHEZWA NA VILABU AU VIKUNDI AU MAKUNDI YA WANANCHI NA MTU MMOJA MMOJA IKIWEMO MAZOEZI, MASHINDANO YA VIWANJANI NA UFUKWENI YOTE YATASUBIRI HADI ITAKAPOTOLEWA TAARIFA NYENGINE HAPO BAADAE.

NDUGU WANANCHI,

TOKEA UGONJWA WA CORONA KURIPOTIWA RASMI HAPA ZANZIBAR TAREHE 18 MACHI, 2020 SERIKALI IMEKUWA IKIFUATILIA KWA KARIBU MWENENDO WA UGONJWA HUO NA HADI KUFIKIA LEO JUMLA YA WAGONJWA 134 WAMETHIBITISHWA KUWA NA MARADHI HAYO, KATI YAO WAGONJWA 109 WAMEPATIKANA UNGUJA NA 25 PEMBA, WAGONJWA 6 KWA BAHATI MBAYA WAMEFARIKI DUNIA TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AWASAMEHE MAKOSA YAO NA AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI - AMIN.

NDUGU WANANCHI,

JUMLA YA WAGONJWA 115 WAMEPONA NA WAGONJWA 19 TU NDIO WANAOENDELEA NA MATIBABU KATIKA KAMBI ZA MATIBABU UNGUJA NA PEMBA, KATI YA HAO, WAGONJWA KUMI (10) WAPO HOSPITALI YA KIDONGO CHEKUNDU, WATATU (3) WAPO SKULI YA SEKONDARI YA JKU MTONI, WAWILI (2) WAPO KIHINANI NA MMOJA YUPO KATIKA KITUO CHA KIDIMNI UNGUJA. KWA UPANDE WA PEMBA KUNA WAGONJWA WATATU AMBO WAPO KATIKA KITUO CHA VITONGOJI. WAGONJWA WOTE HAO WANAENDELA VUZURI NA MATIBABU NA AFYA ZAO ZINAENDELEA KUIMARIKA.

NDUGU WANANCHI,

JITIHADA HIZO ZOTE ZIMEFANIKIWA KUTOKANA NA UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO NA MAIGIZO YA VIONGOZI WETU WAKUU WA KITAIFA AKIWEMO RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI NA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT ALI MOHAMED SHEIN, NICHUKUE NAFASI HII KUWAPONGEZA KWA DHATI VIOGOZI WETU HAO NA TUNAAHIDI KUENDELEA KUFUATA KIKAMILIFU MAELEKEZO YAO KATIKA KUKABILIANA NA MARADHI HAYA.

NICHUKUE PIA FURSA HII KUWASHUKURU KWA DHATI WANANCHI KWA JINSI AMBAVYO WAMEKUWA WATIIFU NA WASIKIVU KWA KUFUATA MAELEKEZO NA USHAURI UNAOTOLEWA NA VIONGOZI WETU PAMOJA NA WATAALAM WA AFYA.

NDUGU WANANCHI,

PAMOJA NA SERIKALI KUREGEZA MASHARTI YALIYOTOLEWA YA KUKABILIANA NA MARADHI HAYA INASISITIZWA KWA WANANCHI KUWA BADO MARADHI HAYA YAPO NA NI TISHIO YANAYOENDELEA KUIATHIRI DUNIA. HATA HIVYO, BAADA YA UZOEFU TULIOKWISHA UPATA WANANCHI SOTE HATUNA BUDI KUPUNGUZA HOFU NA BADALA YAKE SOTE TUENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI STAHIKI ZA KINGA NA MASHARTI YANAYOENDELEA KUTOLEWA NA WATAALAM WA AFYA.

ZANZIBAR BILA YA KORONA INAWEZEKANA

AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA!