- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Zaidi ya Watu 30 wafariki Dunia Naivasha nchini Kenya baada ya Roli la gesi kuripuka
Kenya: Zaidi ya Watu 30 wafariki Dunia Naivasha nchini Kenya baada ya lori lililosheheni gesi kuyagonga magari mengine na kulipuka nje ya mji wa Naivasha Na kuuwa watu zaidI ya 30 na maafisa 11 wa polisi. Inahofiwa huenda idadi ya vifo itaongezeka.
Kwa mujibu wa muakilishi wetu nchini Kenya anaripoti kuwa ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo ( Jumapili).
Pius Masai ambaye ni afisa wa kitengo cha kitaifa kinachoshughulikia majanga nchini Kenya amesema kufikia mwendo wa saa kumi na moja alfajiri, waliokufa walifikia 33. Ameongeza kuwa jumla ya magari 11 yaliteketea kwa moto. Waokozi wanaendelea kupekua eneo la ajali kubaini kama kuna miili zaidi.
Gazeti la Sunday Standard, limesema idadi ya waliokufa inaaminika kuongezeka na kufikia watu 40. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema dereva wa lori hilo, alishindwa kulidhibiti lilipokosa mwelekeo kabla ya kuyagonga magari mengine barabarani kisha likalipuka na kushika moto. Moto huo ukasambaa kwa kasi hadi kushika magari mengine.
Gari la abiria, pamoja na lori la polisi ni miongoni mwa magari yaliyoteketea kwa moto. Maafisa 11 wa polisi wa kupambana na ghasia ni kati ya wale ambao wamefariki kwenye mkasa huo.fanyika usiku wa kuamkia leo
Rais Uhuru Kenyatta amehimiza uchunguzi kamili ufanywe
Rais wa Kenya uhuru Kenyatta kupitia taarifa kwa vyombo vya habari ametaka uchunguzi kamili kufanywa dhidi ya kile anachosema ni ukiukwaji wa sheria inayopiga marufuku malori yanayobeba bidhaa hatari au shehena nyingi kusafiri usiku na katika baadhi ya barabara. Amesema lori lililosababisha ajali hiyo ya kusikitisha halikupaswa kuwa katika barabara hiyo wakati huo wa mkasa.
Kulingana na polisi, lori hilo lililokuwa na nambari za usajili za Uganda, lilikuwa likisafiri kwa mwendo wa kasi na lilikosa mwelekeo pale lilipopita matuta ya barabarani kwa mwendo huo.
Zaidi ya watu 50 waliojeruhiwa kufuatia mkasa huo wamefikishwa katika hospitali ya kibinafsi mjini Naivasha. Walioshuhudia wameelezea kuona moto mkubwa ukiteketeza magari yaliyokuwa na abiria au madereva ndani. Shughuli za kuondoa miili iliyoteketea kupindukia ilianza punde baada ya wazima moto kufaulu kuuzima moto huo.