Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:28 am

NEWS: YOUTUBE, FACEBOOK NA TWITTER ZAPATA HASARA.

Kampuni ya Apple mwaka Jana 2020 ilitangaza itaweka mfumo wa kuzuia apps kukusanya data za app nyingine na kuweka uhuru kwa watumiaji kuwa na uhuru wa kuruhusu app kuwatrack au kuzuia - App Tracking Transparency (ATT) katika iOS 14.

Mfumo wa ATT ulianza rasmi Mwezi wa Nne mwaka huu na ulipingwa sana na Facebook (Meta), Google na platforms za matangazo. Imepelekea kampuni hizo kukosa data za matangazo na data za kufahamu watumiaji wa apps.

Ripoti mpya za The Financial Times zinasema Snapchat, Facebook, Twitter na YouTube mpaka sasa zimepoteza zaidi ya Dola Bilioni 9.85 (sawa na Tshs Trilioni 22.6) kutokana na mfumo mpya wa Apple. Hasara hiyo imepatikana katika kukosa data na kushuka kwa matangazo kwa watumiaji wa iPhone.

Pia imepelekea watumiaji wengi wa Android kupata matangazo mengi kuliko watumiaji wa iPhone kwa sababu Advertisers wanapata impact katika Android kwa sababu inaonyesha matangazo husika kuendana na interests za mtazamaji.