- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WENYE MIMBA RUKRASA KURUDI SHULE
Waziri wa Elimu wa Tanzania Prof. Joyce Ndalichako amesema Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari watakaokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro, mimba na changamoto za kifamilia watapewa fursa ya kurejea Shuleni katika mfumo rasmi huku akitanabaisha kwamba leo Nov 24 , 2021 anakusudia kutoa waraka huo.
"Leo natoa waraka wa elimu ambao utaelezea ni lini wanafunzi watakaokatisha masomo kwa sababu ya mimba na changamoto nyingine watapaswa kurejea shuleni, leoleo natoa waraka hakuna kupoa," amesema Prof. Ndalichako.Aidha Prof. Ndarichako amesema kwamba Wanafunzi wa darasa la 7 wanaofutiwa matokeo kwa udanganyifu na wanaoshindwa kufaulu au wanaopata changamoto zozote wakati wa mitihani watapewa fursa ya kurudia mitihani hiyo mwaka unaofuata.
Leo Profesa Ndalichako amesema uamuzi huo unakwenda kutoa haki kwa wanafunzi ambao kwa sababu hizo walikuwa wamenyimwa fursa.
Kuhusu wanafunzi kurudia masomo amesema shule za Msingi walikuwa wamenyimwa haki kwani wenzao wa kidato cha nne na sita walikuwa na nafasi ya kurudia masomo pale wakishindwa kufaulu mitihani