- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI NDARICHAKO ATANGAZA RATIBA YA MITIHANI
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania Prof.Joyce Ndalichako ametangaza rasmi ratiba ya kufanya mitihani katika ngazi mbalimbali, amesema kuwa mitihani ya Kidato Cha nne itaanza kuanzia Novemba 23 hadi Desemba 11, Kidato cha pili itaanza Novemba 9 hadi 20 na Darasa la saba Octoba 7 hadi 8 na Darasa la nne kuanzia Novemba 9 hadi 20 mitihani yote hiyo inafanyika ndani ya mwaka huu.
Ratiba hiyo imetangazwa rasmi leo Juni 17, 2020 baada ya Rais Dkt John Magufuli kutangaza kufunguliwa kwa shule zote Juni 29 Mwaka huu, Prof Ndalichako amesema ili kukamilisha Muhtasari wa masomo shule zitalazimika kuongeza saa mbili ili kufidia muda uliopotea na ongezeko la muda huo hautahusisha madarasa ya awali.
Pia kuhusu masuala ya ada amezishauri Bodi za shule kukaa kwa pamoja na kuangalia njia ambazo hazitaumiza shule na wazazi na kuwataka wazazi kulipa ada ya muhula wa kwanza Kama hawakulipa lakini shule zisikatae kuwapokea wanafunzi kwa kukosa ada.