Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:33 am

NEWS: WAZIRI MKUU WA SUDAN AJIUZULU

Sudan (MuakilishiTZ). Waziri mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok ametangaza kujiuzulu wadhifa huo. Hamdok ametangaza kujiuzulu jana Jumapili ikiwa ni wiki sita tangu aliporejea madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Oktoba mwaka jana

Bw. Hamdok ametangaza hatua hiyo kupitia televisheni, alisema anaachia wadhifa huo, ili kuruhusu mtu mwingine kusaidia taifa hilo kuvuka katika kipindi cha mpito cha mabadilishano ya kidemokrasia ya madaraka.

Aidha, ametoa mwito wa kufanyika kwa majadiliano ili kufikiwa kwa makubaliano mapya kuhusiana na namna serikali hiyo mpya itakavyofikiwa.

Sudan inapita katika kipindi kigumu kinachotishia mustakabali wa taifa hilo, na kulingana na Hamdok juhudi zake za kuliepusha taifa hilo lisitumbukie kwenye janga zaidi hazikufua dafu.