- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU WA JAPANI APIGWA RISASI
Japan. Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe amepigwa risasi mbili mgongoni na kujeruhiwa vibaya sana alipokuwa katika mkutano wa siasa kwenye mji wa Nara Magharibi mwa nchi hiyo.
Ripoti zinasema kuwa, Abe, alipigwa risasi mara mbili mgohoni na kuanguka chini, huku mshukiwa wa tukio hilo akikamatwa.
Aidha, ripoti zinasema kuwa hali yake ni mbaya na amekimbizwa hospitalini, huku kukiwa na ripoti kuwa haoneshi dalili za kuzinduka.
Abe, aliyeongoza Japan kwa kipindi kirefu kati ya mwaka 2012 hadi 2020, alipigwa risasi wakati akitoa hotuba ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa wabunge siku ya Jumapili.
Shambulio hilo dhidi ya mwanasiasa huyo maarufu mwenye umri wa miaka 67, limewashangaza wengi katika nchi hiyo ya barra Asia ambayo haina historia ya kushuhudia matukio kama haya kufuatia uwepo wa sheria kali za kudhibiti umiliki wa silaha