- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MKUU MAJALIWA AMUOMBEA NAFASI YA PILI ALIYEKOSEA KUAPA
Dodoma. Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amemuombea nafasi nyingine aliyekuwa Naibu Waziri mteule wa Wizara ya Madini Francis Ndulane aliyekosea kusoma kiapo Juzi kwa Rais John Pombe Magufuli.
Waziri Majaliwa amesema anaamini Rais anaweza kumfikiria na kumtafutia mahala akamuaka.
"Yaliyotokea juzi siyo tu Lindi bali tuendele kumuombea kijana wetu,(Ndulane) naamini bado unaweza ukaangaliaangalia, lakini niendelee kusema tu kwamba Wizara ya Madini sasa imepata watu ambao wanaifahamu," amesema Waziri Mkuu Kassi Majaliwa.
"Wizara sasa imepata watu ambao wanaifahamu, eneo hili Mh rais sio eneo la mzaha mzaha sana"
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo Desemba 11, kwenye hafla ya kumuapisha Naibu Waziri wa Madini, Prof.Shukurani Manya aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya, Francis Ndulane aliyeshindwa kuapa juzi na uteuzi wake kutenguliwa.