Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:22 pm

NEWS: WAZIRI MKUU AWAPA SIKU 4 TAKUKURU KUMBURUZA MAHAKAMANI MKURUGEZI TEMEKE

Waziri Mkuu wa Tanzania Kasim Majaliwa amewapa siku 4 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Temeke kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Lusubilo Mwakabibi na wenzake kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika ujenzi wa barabara ya Kijichi Mwanamtoti yenye urefu wa Kilomita 1.8 ikiwa imejengwa kwa gharama ya Bilioni 5.4.

Waziri Majaliwa ametoa maagizo hayo jana Agosti 16, 2021 wakati wa ziara yake katika wilaya ya hiyo ambapo amemuagiza Mkuu wa TAKUKURU Temeke kuwatafuta wahusika wote akiwemo Mkurugenzi huyo wa zamani kwa ajili ya kushitakiwa.

"Nawapa siku 4, tarehe 20 deadline watu waende Mahakamani, ita yeyote yule huyu aliyehamishwa hapa arudishwe, huyo Mkurugenzi aliyewekwa pembeni arudishwe na Msimamizi Msaidizi, Edward Haule rudisha wote peleka mahakamani hatuwezi kufanya mchezo hapa hizi fedha za wananchi”