Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 1:58 am

NEWS: WAZIRI MKUU ATAKA WIZARA KUWEKA UKOMO BEI YA CEMENT

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara, ikamilishe utaratibu mara moja wa kuwa na bei yenye kikomo ya saruji itakayowezesha kila mkoa kujua bei ya bidhaa hiyo, kwa nia ya kuondoa upandishwaji holela unaofanywa na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu nchini.

Majaliwa ametoa onyo pia kwa mawakala wa saruji kutoficha bidhaa hiyo kwa lengo la kupandisha bei kwa sababu kitendo hicho ni sawa na uhujumu uchumi, hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Ameongeza kwa kusema kuwa suala hilo halihitaji kuundiwa bodi kwa sasa kwani vyombo vya kusimamia biashara vipo, wizara husika ipo, hivyo amewataka wahusika wote wahakikishe wanasimamia suala hilo kikamilifu ili kuwawezesha wananchi kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu.

“…Mawakala badilikeni, acheni tabia ya kuficha bidhaa kwa ajili ya kuzipandisha bei, ukikutwa unatengeneza mazingira ya kuifanya bidhaa isipatikane kwa lengo la kuipandisha bei huo ni uhujumu uchumi. Ukikamatwa na bidhaa ambayo inatafutwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa.” ameswma Majaliwa.