- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MBARAWA AANZA KAZI KWA KUTOA MAAGIZO KWA TANROAD
Dodoma. Waziri mpya wa Ujenzi na Uchukuzi nchini Tanzania Prof. Makame Mbarawa amewaagiza Wakala Barabara Nchini (Tanroads) kununua mara moja vifaa vya kupima ubora wa viwanja vya ndege na barabara nchini badala ya kupima kwa kuangalia kwa macho.
Profesa Mbarawa ametoa maagizo hayo hii leo Jumatatu Septemba 13, 2021 muda mchache mara baada ya kuapishwa na Rais Samia wakati wa hafla ya utiliaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.
Mkataba huo ulisainiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (Tanrods) Rogatus Mativila na Kampuni iliyoshinda zabuni ya kujenga uwanja huo ya Synohydro Company Limited.
Awamu ya kwanza ya ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato jijini Dodoma utakaowezesha abiria milioni 1.5 kuhudumiwa kwa mwaka utakamilika baada miezi 36.
Akizungumza Profesa Mbarawa amesema wabunge wamekuwa wakilalamikia kuhusu barabara zinazoharibika baada ya muda mfupi.
“Lakini tukinunua vifaa tutakuwa tunajihakikishia kazi tunayofanya inaenda kwa viwango vya juu. Najua Tanroads mnauwezo mkubwa lakini mkitafuta vifaa vya teknolojia ya juu naamini mtafanya kazi,”amesema
Amesema atalisimamia hilo kwa kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja na nusu kifaa hicho kinafika nchini na hivyo kila barabara inayokamilika iweze kupitishiwa Road Scanner.