- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI MAJALIWA AGOMA KUZINDUZI BARABARA LINDI
Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amegoma kuzindua barabara ya Liwale Mjini ya kilometa 1.2 kwa sababu haijawekwa taa za barabarani kama mkataba wa barabara hiyo unavyoeleza.
Waziri Majaliwa amefanya uwamuzi huo hii leo Octoba 7, 2021 katika siku ya pili ya ziara yake Mkoani Lindi.
“Mkataba ni kujenga barabara za kiwango cha lami zenye taa, leo mnaniambia nizindue barabara haina taa, hii haijakamilika, leo sizindui sababu hamna taa, hayo ni maelekezo ya Rais Samia barabara ya kilometa 1.2 iwe na taa, siku yoyote nitakuja leo siwezi kuzindua”
Taa za barabarani ni moja ya vitu muhimu vinavyopendezesha miji kama inavyoonekana kwenye Miji mbalimbali ikiwemo Lindi mjini kwenyewe ambako kumewekwa taa hizo ambazo licha ya kupendezesha mji, pia zinasaidia usalama na kuruhusu Watu kufanya shughuli zao hadi usiku.