Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 3:34 pm

NEWS: WAZIRI KALEMAN AAGIZA OFISI ZA SEREKALI ZINAZODAIWA KUKATIWA UMEME

Waziri wa Nishati nchini Tanzania Benard Kaleman ameiagiza bodi ya wakurugenzi ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuzikatia umeme mara moja taasisi zote zikiwemo za serikali zinazo daiwa.

Kaleman ameongeza kuwa zoezi la kuwakatia linatakiwa kuanza mara moja na watakao kaidi agizo hilo hatua za kiutendaji zitachukuliwa dhidi yao.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo wakati akizungumza na bodi hiyo makao makuu ya wizara hiyo mtumba jijini Dodoma amesema kuwa serikali inahitaji fedha kwa ajili ya kujenga miradi huku baadhi ya taasisi zikiwa zinadaiwa fedha nyingi.

Katika hatua nyingine Kalemani amesema kuwa Tanesco lazima ijitegemee na hatoomba ruzuku kwa ajili ya shirika hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt.Alexander Kyaruzi ametoa taarifa za maendeleo ya miradi ya umeme ukiwemo mradi mkubwa wa maji wa kuzalisha umeme wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.