- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI GWAJIMA AKIRI KUWEPO KWA MAABUKIZI YA CORONA
Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima amekiri kuwepo na kasi kubwa ya maambukizi ya Ugonjwa wa Corona hapa nchini na kuwataka wananchi wote kuchukua tahadhari na wasisubiri mpaka watu wafe mtaani.
Aidha Dkt Gwajima amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo kila mtu avae barakoa kwenye mikusanyiko, hivyo watu wachukue tahadhari.
“Kasi ya wagonjwa kuendelea kujitokeza na kulazwa kwenye hospitali zetu inaashiria maambukizi yapo, watu wasidhani kwamba tunasubiri mpaka iwe mtaani tunaona maiti ndiyo tuanze kazi, kazi inayofanyika ni kuhakikisha hali haiwi mbaya.
Dk Dorothy Gwajima amesema kuwa watu 408 wamebainika kuwa na ugonjwa wa corona nchini huku 284 wakiwa katika mashine za oksijeni.
“Serikali inajitahidi na Rais amekuwa akikumbusha jamani ndugu zangu tuchukue tahadhari na kujikinga na corona,” amesema Dk Gwajima.
Alitahadharisha kuwa kutokana na kinga ambazo Watanzania wanazo, wasiache kujikinga kwa kuwa wagonjwa wapo na wanaendelea kujitokeza.
“Tunaomba wale ambao hawaitikii tahadhari basi waitikie ili tuongeze wigo ili hali izidi kuwa salama zaidi tusipate idadi kubwa ya wagonjwa, kwenye msongamano vaa barakoa, inawezekana umepona huumwi umebeba unavisambaza, waokoe wengine, kuna wazee na wengine wanaumwa, tukivaa wengi hizi barakoa tunawaokoa wasiovaa,” amesema Waziri Gwajim