- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAZIRI GWAJIMA ACHUKIZWA NA UONGO WA WATUMISHI
Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima amekemea vikali tabia ya watumishi wa sekta ya Afya kuongea uongo na badala yake amewataka kuwa weledi katika utumishi wao ili kutoa huduma bora kwa wananchi siku zote.
Dkt. Gwajima amesema hayo jana wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Nansio Ukerewe Mkoani Mwanza na kubaini kuwepo malalamiko ya uhaba wa dawa kutoka wananchi yaliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Cornel Magembe.
Aidha, Dkt. Gwajima ameshangazwa kusikia wagonjwa hawapewi Paracetamol lakini alivyotembelea stoo akakuta dawa hizo zipo. Pia namna mnyonyoro wa dawa unavyoendeshwa katika Hospitali hiyo umemshangaza Dkt. Gwajima kwani inaonekana kuna uzembe na ubadhirifu mkubwa wa dawa na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali..