Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:18 am

NEWS: WAZIRI ATANGAZA MATOKEO KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA ATOA MAAGIZO KWA MARC NA MADC

DODOMA: Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, amesema kuwa jumla ya wanafunzi 74,166, waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hawajapangiwa shule katika awamu ya kwanza kutokana na uhaba wa madarasa na kuwaagiza wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kukamilisha ujenzi kabla ya Februari 28, 2021.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 17, 2020, jijini Dodoma, wakati akieleza sababu iliyopelekea wanafunzi hao ambao ni sawa na asilimia 8.9, wasipangiwe shule kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.


"Jumla ya wanafunzi 74166 sawa na asilimia 8.9, hawakupangiwa shule katika hii awamu ya kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, ambao hawakupangiwa watapangiwa shule katika awamu ya pili kabla ya Februari 28, 2021", amesema Waziri Jafo.

Aidha Waziri Jafo, amewapongeza viongozi wa mikoa 9 ambao wamefanikisha kupeleka watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

"Jumla ya mikoa 9 ikiwemo ya Kagera, Lindi, Tabora, Songea, Katavi, Mtwara, Mwanza Njombe imeweza kuwapangia sbhule wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kifdato cha kwanza mwaka 20121 nawapongeza viongozi wote wa mikoa hiyo waliofanya juhudi za kuhakikisha wanafunzi wote wanapangiwa".