Home | Terms & Conditions | Help

December 4, 2024, 11:11 am

NEWS: WAWILI MBARONI KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

DODOMA: Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini leo imewafikisha katika mahakama ya wilaya ya Dodoma watuhumiwa wawili kwa makosa ya usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 323 na gramu 69.49.

Mnamo Tarehe 7 novemba 2024 Mamlaka hiyo ilimkamata mshitakiwa Selemani Mbaruku Maarufu kwa jina la Nyanda katika mtaa wa Swaswa Dodoma akisafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 323.

Nyanda anatuhumiwa kwa mashtaka mawili ambapo siku hiyo hiyo pia ya Novemba, 7 katika Mtaa wa Mkomwa Kata ya Viwandani Jijini Dodoma mamlaka ilimkamata akiwa na Kmwaga Msobi wakisafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa gramu 69.49.

Watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya kinyume na kifungu cha 15 kifungu kidogop cha kwanza A cha sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya sura no 95 marejeo ya mwaka 2019.

Kesi hiyo namba 33719 katika mahakama ya wilaya Dodoma inasimamiwa na hakimu Daniel Mpelembwa na wakili wa serikali Meshack Lyaboga, ambapo imeahirishwa mpaka tarehe 16 Desemba mwaka huu na kwa mujibu kesi hiyo aina dhamana na watuhumiwa wataendelea kuwa mahabusu katika kipindi chote cha kesi hiyo katika Gereza la Isanga.