- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATUMISHI WAPYA KUPIMWA AFYA YA AKILI.
DODOMA: Serikali imesema ina mpango wa kuanzisha idara maalum kwenye Sekretarieti ya Ajira kwaajili ya kuwafanyia vipimo vya kisaikolojia watumishi wapya ili kuweza kuwatambua kama wanashida mahala fulani nakuitafutia ufumbuzi kabla hawajaajiriwa lengo kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa weledi.
Hayo yameelezwa Leo Alhamisi Desemba 19,2024 Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa ,Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu wakati akifungua kikao cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu katika Wizara, Idara zinazojitegemea Wakala wa Serikali ,Mashirika na taasisi za Umma, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Sangu amesema hatua hiyo itasaidia kutatua changamoto za baadhi ya watumishi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Aidha amebainisha kuwa kuna mifano mingi ya tabia zisizofaa kazini, ikiwemo watumishi kuonyesha ukaidi, kutokuwa na nidhamu, na kukataa maelekezo kutoka kwa viongozi wao.
“Hivi karibuni nilitembelea halmashauri moja na kukutana na kesi ya mtumishi wa umma, ambaye ni ajira mpya na ana miaka mitatu tu kazini, lakini tayari ameanza kuonyesha ukaidi na kukataa kupangiwa kazi , tabia kama hizi si za kawaida, na mara nyingi huashiria changamoto za kisaikolojia ambazo zinapaswa kushughulikiwa mapema,” Amesema.
Naibu Waziri amesisitiza kuwa utaratibu wa kupima afya ya akili si wa kuminya haki za watumishi, bali ni hatua muhimu ya kuhakikisha watumishi wanakuwa na utimamu wa akili na uwezo wa kushirikiana vyema na wenzao kazini.
Sangu ameongeza kuwa tabia mbaya kazini zinaweza kusababisha migogoro na kushusha morali ya kazi miongoni mwa wafanyakazi wengine, jambo ambalo hatimaye linaathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hata hivyo, Sangu amewataka viongozi wa idara na taasisi mbalimbali za serikali kuhakikisha wanatekeleza sera na taratibu zinazolenga kuboresha mazingira ya kazi, ikiwemo kuwapa mafunzo ya mara kwa mara watumishi ili kuimarisha uwezo wao wa kitaaluma na kisaikolojia.
Ameendelea kufafanua kuwa serikali inahitaji watumishi waadilifu, wachapakazi, na wenye maadili mema ili kufanikisha malengo ya maendeleo kwa taifa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu ,Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Selemani Mkomi amesema katika majadiliano yaliyofanyika katika kikao hicho imebainika kuwa bado kuna changamoto katika masuala ya Utawala wa wasimaminzi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma hususani katika eneo la kutafisri sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kusimamia watumishi wa Umma.
" Katika eneo hili jana kidogo tulichekeshana hapa kwamba kuna watumishi ukiwatathimini unajiuliza kweli walipita kwenye mchakato wa training ya awali kabla hawajaanza kazi, je? Kweli walifanyiwa vipimo vya utimamu kabla hawajaaza kazi kwa sababu kuna mtumishi kama miezi minne iliyopita amekuwa akiandika barua Ofisini kwetu kututuhumu sisi Ofisi ya Utumishi lakini vilevile nakumtuhumu boss wake sababu tu ya uhamisho, ''
''Hajafukuzwa kazi, hajashushwa cheo hajafanyiwa jambo lolote la kumuumiza kwenye utumishi wake ni uhamisho tu wakutolewa eneo moja kwenda eneo jingine kwahiyo mgeni rasmi tulisisitizana mtumishi yoyote anayeajiriwa lazima vipimo vifanyike ili kubaini afya ya huyo mtumishi ili kutokuwa na mtumishi ambaye anaanza kazi bila changamoto, kwa sababu mtumishi huyo kwa taarifa nilizokuwa nazo ni mgeni hana hata miaka kumi lakini tabia alizoonyesha ni zahatari kabisa, "
Kikao hicho cha Wakuu wa Idara kililenga kujadili mbinu za kuimarisha utawala bora, usimamizi wa rasilimali watu, na utoaji wa huduma bora kwa wananchi, huku pia kikitafuta njia za kushughulikia changamoto za utumishi wa umma zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini.