Home | Terms & Conditions | Help

April 6, 2025, 7:25 am

NEWS: WATUMISHI 34 MBARONI KWA WIZI WA MILIONI 307

Waatumishi 34 wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wanashikiliwa na jeshi la polisi Wilayani hapo kwa tuhuma ya upotevu wa fedha za Serekali kiasi cha shilingi milion 307 ambazo zilikusanywa kutoka kwenye vyanzo vya mapato vya ndani.

Inadaiwa baada ya kukusanya, makusanyo hayo hayakuingizwa kwenye akaunti ya halmashauri pia katika kesi hiyo wamo wanaotuhumiwa kufanya malipo bila utaratibu.

Miongoni mwa watumishi hao yumo kaimu mweka hazina Sospeter Makene, aliyekuwa mhasibu wa mapato ya halmashauri hiyo Salanga Mahendeka aliyesimamishwa kazi mwaka 2018, mwingine ni Jastine Banula afisa tehama na Rojas Semkoko afisa tehama aliyesimamishwa kazi mwaka 2018.

Polisi imesema kuwa inaendelea na uchunguzi na watakapokamilisha uchunguzi watawafikisha mahakamani.