- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU ELFU MOJA WAFA KWA TETEMEKO AFGANSTAN
Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa mashariki mwa Afghanstan mapema leo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000. na wengine 1,500 wamejeruhiwa. Hata hivyo, maafisa wamesema iidadi ya vifo inatarajiwa kupanda wakati waokozi wakiendelea na shughuli ya kupekua kwenye vifusi.
Tetemeko hilo la ardhi lililouathiri kabisa mkoa wa Paktika limetokea katika wakati ambao jamii ya kimataifa kwa kiasi kikubwa imeondoka Afghanistan baada ya Taliban kuchukua madaraka mwaka jana kufuatia kuondoka kwa jeshi la Marekani nchini humo. Hali hiyo itafanya juhudi zozote za uokozi na msaada kuwa ngumu katika nchi hiyo yenye idadi ya watu milioni 38.
Kiongozi wa juu wa Afghanistan Hibatullah Akhundzada amesema idadi ya vifo imepanda wakati taarifa zikiendelea kumiminika kutoka maeneo ya milima ambayo sio rahisi kufika.