- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATU 7 WAFARIKI DUNIA KONDOA
Dodoma. Watu 9 wamepoteza maisha mara baada ya Basi la Kampuni ya Emigrace lenye namba za usajili T 703 DLG linalofanya safari zake kati ya Babati na Dar es Salaam, kupata ajali leo Octoba 2, 2021 asubuhi katika mlima wa Kolo, Kata ya Kolo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.
Taarifa za awali zilizotolewa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, watu 7 walipoteza maisha papo hapo ambapo kati yao ni wanaume watu wazima wawili na mtoto mmoja wa kiume, wanawake wawili na watoto wawili wa kike na majeruhi zaidi ya 30.
Baada ya kufikishwa hospitalini majeruhi 2 walifariki Dunia na kufanya idadi ya vifo kufikia 9.
miili ya watu hao imepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Kondoa huku baadhi ya majeruhi wakipelekwa katika hospitali hiyo na wengine wakipelekwa katika Hospitali ya Mrara, Halmashauri ya Mji wa Babati.