Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:35 am

NEWS: WATU 41 WANUSURIKA KIFO AJALI YA BASI MORO

Morogoro. Takribani Abiria 41 waliokuwa wakisafiri na basi la Happy Nation wakitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza, wamenusurika KIFO katika ajali ya gari mara baada ya basi lao kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika eneo la Mkambarani, mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro, ACP Ralph Meela, amesema leo Jumatano July 20, 2020 kuwa chanzo cha ajali hiyo iliyotokea leo ni uzembe wa dereva wa basi aliyeacha njia yake na kulifuata lori hilo.