Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:23 am

NEWS: WATU 14 MBARONI KWA KUSAMBAZA VIDEO ZA MGONJWA WA ICU, MUHIMBILI

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) linamshikilia kijana mmoja jina Allen Samuel Mhina ( 31),ambae ni Mkurugenzi wa Mtandao wa kijamii wa U-turn Collection mkazi wa Temeke Mwembeyanga akiwa na wenzake 13 wanashikiliwa kwa tuhuma za kusambaza video katika mitandao ya kijamii ambayo ni kinyume na sheria.
Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa kusambaza video ikimuonyesha mmoja wa wagonjwa (Polisi hawajamtaja jina) aliyekuwa amelazwa wodi ya ICU Hospitali ya Taifa ya Muhimbili suala lililoleta taharuki kwa Hospitali hiyo na Wafanyakazi wake.

Watuhumiwa hao walikutwa na vifaa mbalimbali vya kieletroniki vya kiuchunguzi ambavyo ni Kamera, Kalamu, Saa Funguo, Miwani, Kofia, Laptop, Memory Card ambavyo vyote vinachunguzwa.

"Kitendo kinachotuhumiwa kufanywa na watuhumiwa hao kililenga kudhalilisha, kutia hofu au kuleta taharuki suala ambalo linalazimisha mamkala hizi mbili za kisheria kuchunguza kwa kina suala hilo, uchunguzi ukikamilika watafikishwa kwenye vyombo vingine vya kisheria"

Itakumbukwa hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi alisema vyombo vya dola vinafanya uchunguzi kubaini aliyemrekodi Prof. Jay (ICU) na akaagiza Hospitali zote nchini kuweka matangazo yanayokataza kupiga picha bila kibali.