- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATATU WAFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI ARUSHA
Arusha. Watu Watatu wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya moramu yaliyopo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika eneo la Kisongo mkoani Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta ametembelea eneo la tukio na kuwaagiza Wataalam wa madini mkoani humo kwenda katika machimbo hayo na kutoa elimu ya njia salama ya kuchimba moramu hiyo.
Mkuu wa mkoa huyo amewataka Wachimbaji wa moramu katika eneo hilo kuendelea na shughuli za uchimbaji huku wakichukua tahadhari juu ya madhara zaidi yanayoweza kutokea.
Amesema amebaini njia inayotumika hivi sasa si salama kutokana na kutokuwa na utaalamu wa kutosha.
Eneo hilo la machimbo ya moramu la Kisongo lina wachimbaji zaidi ya mia tano.