Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:25 pm

NEWS: WATATU WABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

WAKAZI watatu wa Mkoani wa Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam wakikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 1.02.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Yusuph Aboud imewataja washtakiwa hao kuwa ni ni George Mwakang'ata (38) Mkazi wa Mbagala Kuu, Andrew Paul (34) Mkazi wa Kurasini na Said Mugoha (45) Mkazi wa Mtoni Kijichi.