Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 5:04 pm

NEWS: WATATU MBARONI KWA KUMUUA MBINTI YAO KWA KUKATAA KUOLEWA.

Kigoma. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linawashikiilia watu watatu wa familia moja wakazi wa wilaya ya Uvinza mkoani humo, kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua binti yao wa damu wa miaka 17 baada ya kukataa katu katu kuolewa kwa mahari ya Ng’ombe 13.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoani Kigoma ACP James Manyanya amesema hii leo Novemba 12, 2021 kuwa Binti huyo aitwaye Mbaru Juakali alipigwa na fimbo kwa kuchangiwa na watu watatu akiwemo

Mtuhumiwa wa kwaza ambaye ni Baba yake mzazi aitwaye Kurwa Juakali (40), na mwingine ni baba mkubwa wa marehemu Shija Juakali(44), na Baba mdogo Majiba Juakali(29).

"Kwa bahati mbaya sana tukio hili limetokea, tukiwa tunaelekea siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wamtoto, kwahiyo utaweza kuona jinsi jamii bado ipo kwenye ujima, lakini Jeshi la Polisi tunaendelea kutoa elimu ili kuondokana na vitendo hivi vya kikatili dhidi ya watoto" amesema Kamanda Manyanya.

Imeandikwa na Muakilishi Publisher leo Novemba 12, 2021.