- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATANZANIA WAWILI WAKUTWA NA AINAMPYA YA CORONA DENMARK
Watanzania wawili kutoka nchini wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona vya Afrika Kusini walipowasili nchini Denmark kutoka nchini Tanzania.
Taarifa za wasafiri hao zimechapishwa Jumamosi ya Januari 23, 2021 katika ripoti ya taasisi ya utafiti ya kupambana na magonjwa ya kuambukiza, Statens Serum Institut (SSI) imeeleza Wasafiri hao walipimwa tarehe 19 mwezi Januari.
Mpaka siku ya Jumapili, jumla ya watu watatu waliokuwa na maambukizi ya aina hiyo ya kirusi walibainika nchini Denmark. Visa vyote vya maambukizi vimehusishwa na safari.
Juhudi za kumpata msemaji wa serikali na waziri wa afya Tanzania kuzungumzia suala hilo hazijazaa matunda.
Hata hivyo Serekali ya Rais Magufuli imekuwa ikisisitiza kuwa hakuna Corona kwasababu ugonjwa huo uliangamizwa kwa maombi na sala za watanzania.
Tayari nchi ya Uingereza imepiga marufuku wasafiri kitoka nchini Tanzania na Congo kuingia nchini humo kwa hofu ya kueneza ugonjwa huo.