- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WATANO WAFARIKI AJALI YA DALADALA DAR ES SALAAM
kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar ea salaam amesema kuwa Watu watano wamefariki dunia huku wengine 10 wakijeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha basi dogo la abiria na lori la mchanga.
Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo katika eneo la mataa ya Chang’ombe, wilaya ya Temeke, Jijini Dar es salaam.
Kamanda Mambosasa amesema waliokufa ni pamoja na wanaume watatu na wanawake wawili waliokufa papo hapo.
Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, chanjo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kwa kushindwa kuzingatia taa za barabarani.
Kwa mujibu wa mashuhuda, ambao wengine walikuwa sehemu ya abiria kwenye basi hilo lililokuwa linatoka Temeke kwenye Muhimbili, wamesema pamoja na kumsisitiza dereva kuzingatia alama hizo, alipuuza kabla ya basi hilo kugongana na lori kwenye makutano.
Daktari Meshack Shimwela, Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Temeke amesema kuwa wengine wanne waliojeruhiwa walipata huduma ya kwanza na tayari wamepelekwa hospitali ya Muhimbili kwa tiba zaidi huku wengine wakiendelea kupata matibabu katika hospitali ya Temeke.