- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WASAFI FM YAFUNGIWA NA TCRA KWA SIKU 7
Dar es salaam. Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) imesitisha mara moja utoaji huduma za utangazaji kwa kituo cha redio cha Wasafi FM kwa muda wa siku saba kuanzia kesho Septemba 12 hadi Septemba 18 mwaka huu.
Uamuzi huo umetolewa hii leo Septemba 11, 2020 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatua hiyo ni kutokana na kituo hicho kukiuka kanuni namba 11 ya Kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta ya mwaka 2018.
Mhandisi Kilaba amesema kuwa ukiukwaji huo wa kanuni ulifanyika katika vipindi vya The Switch na Mashamsham.
Aidha, ametoa rai kwa vyombo vya habari kuzingatia kanuni za utangazaji wa maudhui yenye lugha ya staha kwa Watanzania huku akiitaka Wasafi FM kuomba radhi kwa umma wa Watanzania.