- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANNE WAKAMATWA KWA KULA NYAMA ZA WATU
Polisi nchini Nigeria katika jimbo la Zamfara kaskazini-magharibi wamewakamata watu wanne wanaodaiwa kuhusika na kula nyama za watu na kuziuza baadhi ya sehemu za binadamu.
Kamishna wa polisi katika jimbo hilo Ayuba Elkanah aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu Gusau siku ya Alhamisi kwamba washukiwa hao walikamatwa baada ya maafisa wa upelelezi kupata maiti katika jengo ambalo halijakamilika huku baadhi ya sehemu za mwili zikiwa zimetolewa.
Ilikuwa ni katika harakati za kufanya uchunguzi wa kupotea kwa mvulana wa miaka tisa. Washukiwa hao wakiwemo wanaume wawili na wavulana wawili walikamatwa wiki iliyopita, kulingana na mkuu wa polisi, na kwamba washukiwa wengine wa genge hilo wanasakwa.
Mkuu huyo wa polisi alisema hadi sasa uchunguzi umebaini kuwa mara mbili kiongozi wa genge hilo aliwalipa washukiwa wengine watatu kiasi cha Naira Laki Tano (sawa na $1,207) kwa ajili ya sehemu za binadamu.
Kuhusika na uuzaji wa sehemu za binadamu na ulaji nyama si jambo la kawaida katika jimbo la Zamfara. Lakini ni moja wapo ya maeneo ya Nigeria yaliyokumbwa zaidi na wimbi la mauaji na utekaji nyara kwa ajili ya fidia na magenge yenye silaha huku mamlaka zikikabiliwa na ukosoaji kwa kushindwa kukabiliana na ghasia hizo.
Hata hivyo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Alhamisi kamishna wa polisi Ayuba Elkanah alisema vikosi vya usalama pia vimewaokoa watu kumi na saba waliotekwa nyara hapo awali kutoka jimbo jirani la Niger na kupelekwa Zamfara.