- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANNE WAFARIKI DUNIA BAADA YA KULA NYAMA YA KASA ZANZIBAR
Zanzibar. Watu wanne wamefariki Dunia hii leo Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar huku wengine 47 wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Kivunge visiwani humo mara baada ya kula nyama ya Kasa inayosadikika kuwa na sumu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi Unguja Mathias Otieno amesema kuwa kunamvuvi mmoja kwa jina la Juma Juma Ncha alimuona kasa akiwa ufukweni akitaga mayai katika eneo la Madomwe ngulumaji akawaita wavuvi wenzake kusaidiana kumshika kasa huyo. Baada ya kumshika walimchinja na kugawana nyama.
Kamanda Otieno amesema Wavuvi hao Wakapeleka nyama hiyo kwenye familia zao kwaajili ya kitoweo ndipo mmoja akafariki Dunia mara tu baada ya kutumia nyama hiyo ambaye ni Amiri Juma Juma mtoto wa mvuvi huyo.
"Baadae ikapelekea watu kama 50 wakaanza kujisikia vibaya, baadae wakawa wamekimbizwa katika hospitali ya kivunge kwa ajili ya matibabu, wakati wakiendelea kupatiwa matibabu watatu kati ya hao 50 wakafariki Dunia ambao ni Zainabu Juma Juma(1), Makame Ally Juma(4), na Dawa Juma Ncha (6). "
Kamanda Otieno amesema kuwa katika hao watu 47 wanaoendelea kupatiwa patibabu 38 ni watoto kuanzia umri wa miaka 18 kushuka chini na 9 ndio watu wazima.
Imechapishwa na Muakilishi Pulisher
Desemba 25, 2021