- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAUME WAILILIA SERIKALI YA KIJIJI KUNYIMWA UNYUMBA NA WAKE ZAO.
MLODA DODOMA: Katika Kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia Mwenyekiti wa Kijiji cha Mloda Kata ya Mlowa barabarani Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Adam Philimon, amesema miongoni mwa malalamiko yaliyokithiri katika Kijiji hicho ni wanaume kunyimwa ujumba.
Philimon, amesema hayo wakati kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyoendeshwa na shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid Tanzania kupitia Mradi wa TIF (Transformative Impact Fund) yenye lengo la kuendeleza kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabia nchi (Kilimo ikolojia) kwa wakulima wadogowadogo hasa Wanawake na Vijana.
Amesema kunyimbwa unyumba ni miongoni mwa kesi anazopokea katika ofisi yake na hali hiyo imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa migogoro ya ndoa na nyingine kuvunjika kabisa, huku akiwataka wanaume kutoa taarifa za vitendo hivyo kwenye sehemu husika ili kutokomeza janga hilo.
"Wanaume wanaogopa tu kusema hapa lakini matukio ambayo tumekuwa tukiyapokea hapa kijijini kwetu ni wanaume wengi kunyimwa unyumba na wake zao unakuta mtu anasema mwenyekiti mimi mke wangu kila nikihitaji ananikatali,''
" Na kunakesi moja ya mwanamke alikua hampi mume wake unyumba na haki hiyo anampatia mtu mwingine ambaye siyo mume wake yaani ni kama anaishi na mume lakini unyumba anapewa mtu mwingine", Amesema
Aidha amesema matukio mengine ya wanaume kunyanyaswa na wake zao wenye vipato hasa mwisho wa mwaka ambapo akina mama wengi wanavunja vikoba vyao.
"Mwezi huu wa Disemba wakati akina mama wanavunja vikoba vyao tumekuwa tukipokea malalamiko mengi ya wanaume kunyanyaswa na wake zao sisi kama serikali tunayapata sana malalamiko haya kutoka kwa wanaume wengi" Amesema.
Vile vile, amesema malalamiko mengine ni watoto wa kike kuodheshwa katika umri mdogo na kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo kusoma ''Mbali na hayo kwa upande umiliki wa ardhi kwa wanawake hakuna upendeleo kwa watoto wa kiume wala wakike wote wanapata kwa uwiano sawa,''
Akizungumza kwa niaba ya Wanawake wa Kijiji cha Mloda Mariam Mahajile amesema sababu zinazopelekea wanaume kufanyiwa ukatili huo ni wanaume kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa na kuchoshwa na majukumu yakutafuta riziki nakukosa hamu ya tendo hilo ikiwa baadhi yao kulekeza familia nakuwachia wao kulea familia.
"Siyo kama hatutaki Kuwapa unyumba wanaume lakini pia wao hawatupi mapenzi ilivyokuwa awali wanatubaka hawatufikishi kule tunakohitaji kufikishwa" Amesema
Mbali na hayo ametaka elimu jumuishi izidi kutolewa kwa jamii kuhusu vitendo hivyo na serikali kutofumbia macho na ichukue hatua kwa watuhumiwa wa ukatili huo, nakuongeza kwa kuvitaka vyombo vya maamuzi kutenda haki kwa wahanga katika kushugulikia janga hilo.
Kwa upande wake Mhasibu wa Jukwaa la Wakulima Wanawake Wilaya ya Chamwino Nuru Mpanda amewahimiza wanawake kuwaheshimu Waume zao hata kama wanavipato vikubwa vyakuwazidi wao.
"Mwanamke hata kama wewe ndiye unayeleta hela kwa ajili ya matumizi ya ndani lazima uwe na heshima kwa muwe wako siyo unarudi usiku halafu ukipigwa unasema nipige nikupeleke kwa wanaume wenzako, "
Naye Mratibu wa Mradi wa TIF (Transformative Impact Fund) Kutoka Shirika la Actionaid Tanzania Happy Itrosamesema mradi huo unatekelezwa katika nchi nne ambazo ni Rwanda, Burundi, Tanzania na DRC , Kwa Tanzania upo Mikoa miwili Dodoma na Singida na Dodoma uko wilaya ya Chamwino katika vijiji kumi ambavyo ni Mlowa Barabarani, Mloda, Nzali, Kawawa, Msanga, Iringa Mvumi, Makang'wa, Chinangali II, Chamwino na Mahama.
Lengo la mradi TIF ni kuwawezesha wakulima kupaza sauti za changamoto zao kwa kushiriki katika kutengeneza suluhisho kupitia majukwaa mbaimbali ya kijamii , pia kuchanganua sera na mipango mbalimbali zinazochangia kilimo ikolojia.