Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 3:07 pm

NEWS: WANASHERIA MKUU WA SEREKALI AWATETEA KINA HALIMA MDEE

Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Profesa Adelardus Kilangi amekionya chama kikuu cha Upinzani nchini humo CHADEMA kutowabugudhi wabunge wake wa chama hicho wa viti maalum.

Profesa Kilangi ametoa kauli hiyo Jana wakati akifanyiwa mahojiano na gazeti la chama tawala CCM la Uhuru huku akisema, kwamba mchakato wa Wabunge wa viti Maalum kutoka CHADEMA umefuata Sheria na Katiba, hivyo hawapaswi kubugudhiwa.

Awali Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai alisema, kanuni za bunge zinamtaka kuwalinda Wabunge walio wachache na maslahi yao na kuahidi kufanya hivyo kwa nguvu zake zote.

Ndungai alisema wabunge hao 19 wameteuliwa kihalali na kama CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala ya kuwahukumu.Amesema majina ya wabunge wa viti maalum alipewa na na Tume ya Uchaguzi, na kazi yake ni kuwaapisha Wabunge hao na ameshafanya hivyo.