- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAOMILIKI SILAHA KIMAGENDO WAPEWA SIKU 30
Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amewapa siku 30 watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha Polisi ndani ya muda huo ili wasichukuliwe hatua kali za kisheria.
Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 30, 2021, Simbachawene amesema shughuli hiyo ya kusalimisha silaha itaanza Novemba Mosi hadi Novemba 30, 2021.
“Kupitia tangazo la Serikali namba 774 la Oktoba 29, mwaka huu natangaza msamaha wa kutoshtakiwa kwa wale watakaosalimisha silaha kwa hiari kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa kwenye tangazo,” amesema Simbachawene.
Amesema silaha hizo zisalimishwe katika vituo vyote vya jeshi hilo nchini na ofisi za Serikali za mitaa na kwa watendaji wa kata kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10 jioni.