- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANANCHI WA URUSI WAPIGA KURA KUTWAA MAENEO YA UKRAINE
Wananchi wa Urusi wameanza leo ASUBUHI kupiga kura ya maoni katika maeneo inayoyakalia baada ya kuyatwaa mashariki na kusini mwa Ukraine ili kuamua kama mikoa hiyo itaunganishwa na Urusi au la.
Mikoa minne tayari imetangaza kuanza kwa zoezi la upigaji kura itakayofanyika kuanzia leo hadi Jumanne wiki ijayo katika mikoa minne ya Luhansk, Donetsk, Kherson na Zaporizhzhia, inayowakilisha karibu asilimia 15 ya ardhi ya Ukraine.
Mamia kwa maelfu ya watu wataweza kupiga kura hadi Septemba 27. Mkoa wa Luhansk umetangaza kuwa raia ambao wamekimbilia Urusi wataweza kupiga kura wakiwa huko.
Kiongozi wa wanaotaka kujitenga na Ukraine huko Donetsk Denis Pushilin ameizungumzia siku hii kama muhimu na ya kihistoria na kusema huu ndio uhalisia wa sasa.
Urusi inataka kutumia matokeo ya kura hiyo ya maoni ili kuyaunganisha maeneo hayo kwa kigezo cha "haki ya watu kujiamulia wenyewe". Ukraine na hata jumuiya ya kimataifa zimetaja kutoitambua kura hiyo wakati Urusi wakiikalia kimabavu ardhi ya Ukraine.
Je Kura hiyo ya maoni ni halali ?
Kura hiyo ya maoni haizingatiwi kama ni halali kwa sababu inafanyika bila ya ridhaa ya Ukraine, chini ya sheria ya kijeshi na si kwa mujibu wa kanuni za kidemokrasia. Lakini pia waangalizi wa kimataifa hawawezi kufanya kazi yao kwa uhuru. Matokeo yenye upendeleo kwa Urusi yanatarajiwa kuwa na athari kubwa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu kura hiyo ya maoni huku akiwapongeza washirika wa Magharibi kwa kulaani hatua za Urusi. Wananchi pia wa Ukraine wanaipinga kura hiyo kama anavyoeleza Tatiana ambaye ni mkimbizi wa ndani kutoka Kherson:
"Ninapinga kura ya maoni. Nadhani mji wetu na eneo letu ni mali ya Ukraine. Hii ni hali ngumu mno na ninafikiri hakuna nafasi ya Warusi katika ardhi yetu."
Kura hiyo inajiri baada ya Ukraine mwezi huu kuyakomboa tena kwa wingi maeneo yake baada ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza, ikiwa ni miezi saba tangu Urusi kuivamia na kuanzisha vita vilivyoua maelfu ya watu, na kupelekea mamilioni ya wengine kuyakimbia makazi yao na kuvuruga uchumi wa dunia.
Wiki hii Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza rasimu ya jeshi ya kuwasajili wanajeshi wapya 300,000 ili kushiriki vita vya Ukraine, katika harakati za Moscow kujaribu tena kuudhibiti mzozo huu.