- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANANCHI KUKOSA HUDUMA YA LUKU KWA SIKU NNE
Dar es Salaam. Shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) limesema kuwa kutakuwa na ukosefu wa ununuaji wa Umeme kwa njia ya Luku kwa siku nne, mfululizo yaani kuanzia Septemba 12-15, 2022 na ni kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kinga kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Septemba 5, 2022 na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imebainisha kuwa wakati huo wa matengenezo ambayo yatafanyika usiku wateja hawataweza kupata huduma hiyo.
“Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linapenda kuwataarifu wateja wake wa malipo ya awali (Luku) kuwa kutakuwa na matengenezo kinga kwenye kanzi data ya mfumo wa manunuzi ya umeme (Luku)
“Zoezi hili linatarajiwa kuchukua siku nne Jumatatu Septemba 12 hadi 15, 2022 ambapo wateja wetu wataweza kununua umeme wakati wote isipokuwa wakati wa matengenezo kwa vipindi vifupi nyakati za usiku” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Shirika hilo limewashauri watumiaji wa huduma hiyo kununua umeme wa ziada au kufanya manunuzi nje ya muda wa matengenezo.