- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANANCHI KUANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Dodoma. Serekali imesema imeanza kuchapisha vitambulisho vya taifa na kuvisambaza katika ofisi za wilaya nchi nzima, mara baada ya zoezi hilo kusitishwa kwa miezi kadhaa.
Kauli hiyo ya Serekali imetolea na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamza Chilo akiliambia Bunge kuwa zoezi la uchapishaji vitambulisho lilikwama na kuchelewesha usambazaji “hata hivyo serikali bado haijashindwa kuwapatia wananchi vitambulisho.”
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Paresso aliyehoji ikiwa serikali imeshindwa kuwapatia wananchi vitambulisho hivyo, Chilo alisema zoezi la usambazaji vitambulisho katika wilaya limeanza.
Hakusema idadi ya vitambulisho vilivyochapishwa hadi sasa, hata hivyo alisisitiza kasi ya uchapaji vitambulisho sio ya kawaida na kwamba wananchi watapata haki yao ya kuwa na vitambulisho vya taifa.
Paresso alidai kuwa idadi kubwa ya wananchi wamekuwa na namba ya utambulisho bila kuwa na kadi kwa karibu miaka minne sasa.