- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANAFUNZI WAIBANA HALMASHAURI YAO.
DODOMA: Club za Wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari wameiomba Halmashauri ya ya Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma kuitupia jicho sekta ya Elimu katika bajeti ijayo 2022/2023 ili kupunguza changamoto 10 zinazowakabili Wanafunzi hususani shule za msingi .
Miongoni mwa Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa Matundu ya vyote, ukosefu wa vyumba vya faraga, uhaba wa Maji mashuleni, ukosefu wa nyumba za Walimu, upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi katika shule za Sekondari, Na miundombinu mibovu kwa wanafunzi wenye mahitaji Maalum.
Akiwasilisha mapendekezo kwa uongozi wa Halmashauri katika mkutano wa wadau wa elimu uliondaliwa na shirika lisilo la Kiserikali la Actionaid Tanzania Mwenyekiti wa Club za Wanafunzi mashuleni ambaye pia ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlowa Wema Nollo amesema,,
‘’Unakuta shule moja inawanafunzi zaidi ya elfu moja na inamatundu sita wasichana matatu na wavulana matatu, muda wa mapumziko ni dakika 20 wanaoenda kujisaidia ni wengi ,na msongamano ni mkubwa namuda muda wa vipindi unakuwa tayari umefika hii husababisha kuchelewa vipindi na wakati mwingine inasababisha kupata magonjwa kama uti,’’
Akizungumzia changamoto ya umbali wa shule kwa wananfunzi , Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Buigiri Chamwino Editha Mabwe ameiomba Serikali kuwajengea mabweni au shule karibu na vijiji ilikupunguza utoro na kukuza taaluma katika halmashauri hiyo.
‘’Shule nyingi za Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino zimejengwa mbali na makazi ya Kijiji kwa mfano Chilonwa, kuna wanafunzi wanatoka Mlimwa wanakuja kusoma shule ya sekondari Chilonwa,
‘’Kuna wanafunzi wanatoka Kijiji cha Chiwahele wanakuja kusoma Buigiri, hali ile inawasababishia wanafunzi kupata changamoto mbalimbali ikiwemo wasichana kubakwa,,’’amesema Mabwe.
Akipokea mapendekezo hayo kwa niaba ya madiwani, Mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo Edson Sweti amesema wameyapokea mapendekezo hayo nawatayafanyia kazi kwa uharaka na kwawakati ili kutatua changamito hizo.
‘’Tutaa tushauriane na wenzetu hawa ili asilimia kubwa ya bajeti iende kwenye matundu ya vyoo, tunapotoka hapa tunaenda kuyafanyia kazi kwa kuwa changamoto hizi zimeanzia nyuma huko,’’amesema mwenyekiti huyo.
Afisa Elimu Sekondari Wilaya hiyo Tulinagwe Ngonile Alikiri kuwepo kwa changamoto hizo na nakuahidi kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamejipanga kutatua changamoto zote zilizopo.
‘’Hivi sasa hivi tunamiradi mbalimbali katika ngazi ya Sekondari tuna mradi wa kuboresha elimu ya sekondari, kupitia mradi huu tutaenda kufanya ujenzi wa miundombinu , tutajenga shele mpya lakini pia tutaongeza miundombinu kama vile maabara , vyoo na madarasa kwahiyo hii changamoto ya vyoo sasa itakuwa historia ,’’ amesema Ngonile.
‘’Mfano kwenye bajeti yetu ya mwaka wa fedha ujayo tunajumla ya madarasa 53 ambayo tumetengewa kwaajili ya shule zetu za Msingi hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani, pia kwenye mradi wetu wa busti tunajumla ya matundu ya vyoo 150 katika shule zetu za msingi tumeelekeza kupeleka katika shule zenye changamoto,’’ amesema Afisa Elimu Vifaa na Takwimu idara ya Elimu Sekondari wilaya ya chamwino Mwl Nyemo Masimba.
Mradi wa boresha elimu katika Mikoa ya Singida na Dodoma chini ya ufadhili wa shirika la AtionAid Tanzania unalengo la kuchochea na kuikumbusha Serikali kutatua changamoto zinazozikali shule za sekondari namsingi ili kukuza taaluma nchini.