- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WALIOMUUA KADA WA CHADEMA MAWAZO WAHUKUMIWA KIFO
Mahakama Kuu kanda ya Mwanza imewahukumu adhabu ya Kifo Alfan Apolnari, Epafra Zakaria, Hashim Sharifu na Kalulinda Bwire mara baada ya kutiwa hatiani kwa kumuua kwa kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita na Kanda ya Ziwa, Alphonce Mawazo.
Mawazo aliuawa kikatili kwa kukatwa katwa na vitu vyenye ncha kali Novemba 14, 2015 na mwili wake kukutwa pembezoni mwa barabara.
Mawazo aliuawa siku chache baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Katika uchaguzi huo Mawazo aligombea ubunge jimbo la Busanda.
Desemba 14 mwaka huu mahakama hiyo iliwakuta na Kesi ya kujibu washtakiwa hao.
Katika shauri lao namba tisa la mwaka 2019, mshatakiwa wa nne, Habibu Feruzi ameachiwa huru baada ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kushindwa kuthibitisha kuhusika kwake kwenye mauaji hayo ya kukusudia hivyo kutokuwa na kesi ya kujibu.
Hakimu mwandamizi mwenye mamlaka ya juu kusikiliza kesi ya mauaji, Frank Mahimbali ameieleza mahakama kuwa baada ya kuitafakari kesi yote na kusikiliza upande wa mashtaka na mashahidi 13 pamoja na vielelezo vitano na ushahidi, mahakama imewakuta na kesi ya kujibu washtakiwa wanne.