Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 5:14 pm

NEWS: WALIOMSHAMBULIA LISSU KWA MAWE WAKAMATWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Emmanuel Lukula amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 12 wanaodaiwa kufanya vurugu za kushambulia kwa mawe, mkutano wa mgombea Urais wa chama cha upinzani Chadema Tundu Lissu Wilayani Hai siku za hivi karibuni.

"Tumetumia sana intelejensia ya Polisi ili kuwabaini hao watu waliofanya kitendo hicho cha aibu kubwa tumefanikiwa kuwapata 12, wengine tumewakamatia Arusha wanasema baada ya hilo tukio waliona kama wangerudi majumbani mwao wangekamatwa, tumewafuatilia kwa muda mrefu lakini tumeona tuwafuate walipo, mbaya zaidi wanatueleza kuwa kuna mtu aliyekuwepo nyuma yao na amekimbia" amesema Kamanda Lukula leo Agosti 23, 2020

Agosti 14 mwaka huu Lissu alikwenda Mkoani Arusha kusaka wadhamini ili kukidhi masharti ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Sheria za Uchaguzi zinavyotaka, kuwa lazima upate wadhamini 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania.

Wakati Lissu na Msafara wake wanakaribia kufika kwenye Ofisi za Chama chake cha Chadema wilayani hai, alishambuliwa kwa mawe na genge la watu walioibuka ndani ya msafara huo.

Aliyekuwa Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter alitoa taarifa punde baada ya tukio hilo kuwa msafara wa Tundu Lissu umevamiwa katika Ofisi za Chama hicho Wilayani Hai

"Msafara wa mgombea Urais Mh Tundu Lissu umevamiwa na kushambuliwa vibaya katika ofisi ya CHADEMA HAI,magari yame haribiwa. Mgombea Uraisi na Team yake wako salama. Polisi wako lakini wana shuhudia, mkutano umevunjika. Alisema Lema