- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WALIMU 201,707 KUFANYIWA USAILI.
DODOMA: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene amesema jumla ya Walimu 201,707 wanatarajiwa kufanyiwa usaili kuanzia Januari 14 hadi Februar 24, mwaka huu kwa ajili ya kujaza nafasi 14,648 zilizo tangazwa na serikali, ili kupunguza uhaba wa walimu nchini.
Simbachawene amebainisha hayo leo Jumamosi Januari 11,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu usaili huo.
Amesema “Kuanzia tarehe 14 Januari hadi terehe 24 Februari, 2025, usaili wa kada za Ualimu utaendeshwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (UTUMISHI), Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Afya, Tume ya Utumishi wa Walimu, Ofisi za Wakuu wa Mikoa yote na wataalamu mbalimbali kutoka katika Taasisi za Umma," amesema.
Aidha, Simbachawene, amesema usaili huo una lengo la kujaza nafasi 14,648, zilizotolewa na Rais kwa lengo la kupunguza uhaba wa walimu nchini.
“Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwasihi sana wale wote walioitwa kwenye usaili wajiandae vyema kwa usaili huo kwani nafasi hizi ni za ushindani.
“Vilevile, kulingana na mahitaji yetu ya elimu kwa sasa, tutaajiri wataalamu wa fani za Amali, hivyo, nawasihi sana wale wote watakaopata nafasi ya kuajiriwa, wawe tayari kujiendeleza ili kuweza kukidhi matakwa ya ajira zao katika Utumishi wa Umma,”amesisitiza
Amesema usaili huo wa kada za ualimu utafanyika katika Mkoa ambao kila msailiwa anaishi lengo ni kuwapunguzia gharama za kusafiri na mambo mengine.
“Sekretarieti ya Ajira ilitoa matangazo kumtaka kila msailiwa kuhuisha taarifa zake katika akaunti yake ya Ajira Portal sehemu iliyoandikwa ‘current physical adress’ kwani ndipo tumewapangia vituo vya usaili kulingana na anuani walizojaza,”amesema
Pamoja na hayo amewasihi waombaji wote kuhakikisha kila mmoja anakwenda katika kituo ambacho amepangiwa kwa ajili ya usaili kwani mahitaji yake ya msingi yapo huko.
Vile vile, amesema usaili wa awali wa kuandika (Mchujo) kwa kada za Ualimu utafanyika kwa njia ya kuandika kwa mkono kwa kada zote na ngazi zote za elimu.
“Ninapenda kuwakumbusha wale wote watakaokwenda kwenye usaili wahakikishe wanabeba vyeti vyao halisi kikiwemo cheti cha taaluma na cheti cha kuzaliwa,”amesema.
Mwisho