Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 10:03 pm

NEWS: WAKUFUNZI 8 CHUO CHA RUCU MBARONI KWA UDANGANYIFU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nnchini Tanzania (TAKUKURU) mkoa wa Iringa imewafikisha mahakamani watuhumiwa nane kwa makosa 480 ya udanganyifu na kujipatia zaidi shilingi milioni 500 kutoka Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU) kilichopo mjini Iringa.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Iringa,- Mweli Kilimali amesema watuhumiwa hao wametenda makosa hayo kati ya mwaka 2014 na 2019, wakifanya kazi ya kufundisha RUCU huku wakijua ni waajiriwa wa Serikali, hivyo kupata mishahara miwili kinyume na sheria za utumishi.

Washtakiwa wote wamerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.