- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKILI WA MBOWE ASHINDWA KUJIZUIA KWA FURAHA
Dar es Salaam. Kiongozi mkuu wa jopo la mawakili waliokuwa wakimtetea Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Peter Kibatala amejawa na furaha na kububujika na machozi ya furaha yake baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kufuta kesi iliyokuwa ikiwakabili wateja wao na kuwaachia huru.
Akizungumza leo Machi 4 nje ya Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam, Kibatala amesema walifika mahakamani hapo wakiwa wamejiandaa kwa ajili ya utetezi.
“nianze kwa kushukuru jopo la mawakili ambao pamoja nami walipigana kiume na kike kwa kutegemea jinsia zao. Tanzania na dunia nzima imeshuhudia hakuna kitu chochote tumekiacha, tumetoa jasho, damu na mioyo yetu" kibatala
“tunafurahi wateja wetu waliokaa muda mrefu wametoka,ukitoa Mbowe ambaye amekaa miezi tisa gerezani,wale vijana ambao wameitumikia nchi yao kwa jasho na damu kwenye mazingira ambayo dunia imesikia wamewekwa gerezani,”
“Leo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kwa kutumia madaraka yake aliyopewa na sheria inayoongoza namna ya kuendesha kesi za Jinai nchini amewasilisha mahakamani hati ya nia ya kutoendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa wote.
“Mnakumbuka walikuwa wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali chini ya mwamvuli wa uhujumu uchumi lakini makosa yenyewe yalikuwa makosa yanahusu ugaidi. Mtakumbuka kwamba shauri hilo lilikuwa limepangwa leo kwa ajili ya utetezi.
“Sisi tulikuwa tumejipanga kwa ajili ya utetezi, kwa hiyo sisi tunafurahi kwa hatua hiyo tulitimiza wajibu wetu kwa kadri ya Mungu alivyotuongoza wote. Ambao mlifuatilia mliona kwamba tulifanya kila kile ambacho Mungu ametujalia katika ujuzi wa sheria. Nchi nzima na dunia nzima imeona sisi tunafurahi kwa sababu yetu na kwa sababu ya kazi ya mikono yetu” Kibatala